Mambo Yasiyosemwa Kabisa Kuhusu Upekee wa Kakakuona, bonyeza kwenye link hii kusoma makala nzima
https://wildlifetanzania.co.tz/mambo-yasiyosemwa-kabisa-kuhusu-upekee-wa-kakakuona/
Muendelezo wa Makala;
Bahati nzuri, Taasisi ya Utafiti na Uhifadhi Tanzania, Tanzania Research and Conservation Organization (TRCO) imeanza kuonyesha njia kwenye jambo hili nyeti. Taasisi hii ya TRCO, inafanya tafiti za kina kujua mambo yote ya msingi kuhusu kakakuona waliopo Tanzania, idadi yao, biashara, changamoto zinawapata wanyama hawa, njia sahihi za kuwabeba, sehemu sahihi za kuwaachia endapo watakuwa wamekamatwa maeneo ya makazi ya watu nk.
TRCO inashirikiana na Mamlaka na Taasisi za Serikali, Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania, kuhakikisha tafiti za kina kuhusu kakakuona zinafanyika. Pamoja na mambo mengine ya utafiti, TRCO imejipaga kuandaa program za kuelimisha, kutoa mafunzo kwa wahifadhi na jamii kuhusu namna bora ya kuhifadhi kakakuona wa Tanzania.